Shambulio la droni laripotiwa katika makao makuu ya televisheni Tigray

Shambulio la ndege isiyo na rubani limegonga makao makuu ya kituo cha televisheni cha Tigray TV, mjini Mekelle, kaskazini mwa Ethiopia, na kulazimisha kusitishwa kwa matangazo.

Wakati hayo yakijiri, shambulio la ndege isiyo na rubani imelenga makao makuu ya kituo cha televisheni cha Tigray TV, mjini Mekelle, kaskazini mwa ncho hiyo.

Picha kutoka eneo la tukio zinaonesha sehemu kubwa ya jengo hilo la utangaziaji likiwa limeharibiwa na madirisha yakivunjika vibaya. 

Wanahabari wa kituo hicho wamesema shambulio hilo lilitokea Jumapili majira ya saa tatu asubuhi, wakati matangazo yakiendelea.  Wiki iliyopita, serikali jijini Addis Ababa ilitangaza kufungwa kwa Televisheni hiyo.

Hata hivyo, bado haijabainika ni nani aliyehusika na shambulio hilo wala sababu iliyolengwa. Hili ni tukio linakuja wakati huu TPLF na makundi mengine yenye silaha, yakiendelea kusonga mbele zaidi, Kaskazini mwa Ethiopia.

TPLF imesema imechukua udhibiti wa baadhi ya viwanja vya ndege na kuanzisha mashambulizi katika majimbo jirani ya Afar na Amhara, ikidai kuwa inajibu kile ilichokiita uchokozi wa Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed.

Mkataba wa amani wa Pretoria, uliotiwa saini mwaka 2022 na kuungwa mkono na Umoja wa Afrika na Marekani, kwa kiasi kikubwa hujawahi kutekelezwa na wasiwasi wa kuzuka tena kwa vita ulianza kushuhudiwa tena mwaka uliopita.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii