Msanii wa Nigeria, Davido, ameibuka kuwa msanii mwenye uteuzi mwingi zaidi katika tuzo za AFRIMMA 2026 baada ya kutajwa katika vipengele vitano.
Davido ametajwa katika vipengele mbalimbali ikiwemo Artist of the Year, Best Male West Africa, Crossing Boundaries With Music Award na AFRIMMA Album of the Year kupitia albamu yake 5ive.
Ushirikiano wake na Omah Lay kupitia wimbo With You umeingia kwenye vipengele vya Best Collaboration na Song of the Year, jambo linalompa nafasi ya kushinda tuzo zaidi ya moja.
Tuzo za AFRIMMA zimerejea mwaka huu baada ya kusimama kwa kipindi cha miaka miwili. Waandaaji pia wameongeza AFRIMMA Music Festival, itakayofanyika sambamba na hafla ya utoaji wa tuzo mjini Dallas, Texas, Marekani.
Hafla hiyo imepangwa kufanyika Septemba 12, 2026, katika Annette Strauss Square, Dallas.
Mbali na Davido, wasanii Burna Boy, Diamond Platnumz na Black Sherif wamepata nominations nne kila mmoja, hivyo kuongeza ushindani katika tuzo hizo za muziki wa Afrika.