Korea Kaskazini yasisitiza uungaji wake mkono kwa Urusi

Korea Kaskazini imesisitiza uungaji wake mkono kwa vita vya Urusi nchini Ukraine wakati wa mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi hizo mbili yaliyofanyika mjini Moscow.

Shirika la Habari la Korea Kaskazini limeripoti kwamba Waziri Choe Son Hui na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov wamekutana kwa mara ya tatu hapo jana Jumatatu kwa lengo kuendeleza mashauriano ya pande mbili hasa katika wakati usuhuba baina ya mataifa hayo mawili unaimarika.

Taarifa zinasema Waziri Hui ameelezea uungaji mkono usioyumba kwa sera za ndani na nje za Urusi katika kumaliza chanzo cha mzozo wa Ukraine.

Korea Kaskazini ilituma wanajeshi kadhaa kwenye mkoa wa Kursk kuisaidia Urusi kwenye vita vya Ukraine na imeipatia pia Moscow mifumo kadhaa ya ulinzi kwa ajili ya vita vinavyoendelea.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii