Maelfu ya wahamiaji usiku wa kuamkia leo hii walivuka kutoka Morocco kuingia katika eneo la Ceuta linalodhibitiwa na Uhispania katika Afrika Kaskazini.
Maelfu ya wahamiaji usiku wa kuamkia leo hii walivuka kutoka Morocco kuingia katika eneo la Ceuta linalodhibitiwa na Uhispania katika Afrika Kaskazini, chanzo cha polisi kimesema leo hii, kikiongeza kuwa haikuwezekana kukadiria idadi kamili ya watu waliovuka mpaka huo.
"Kulikuwa na wimbi kubwa la watu lililokuwa likiendelea usiku mzima," chanzo hicho kikiongeza kuwa ingawa idadi ya waliowasili ilikuwa ndogo ikilinganishwa na ile ya mchana, wahamiaji waliendelea kuwasili usiku kucha na bado walikuwa wanaingia eneo hilo hadi Asubuhi ya leo.
Chanzo hicho kimesema jumla ya watu 18 walifariki duniawalipokuwa wakijaribu kufika katika eneo hilo la Uhispania.