Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa mchezo wa Ngao ya Jamii kwa msimu wa 2026/27 utachezwa katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mchezo huo wa ufunguzi wa msimu mpya wa soka nchini Tanzania utawakutanisha watani wa jadi, Young Africans SC na Simba SC, katika pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo Julai 31, 2026, mchezo huo umepangwa kuchezwa Jumatano, Agosti 12, 2026, kuanzia saa 2:30 usiku kwenye dimba la Amaan, Zanzibar.
Ngao ya Jamii hiyo itakuwa mwanzo rasmi wa msimu wa 2026/27, huku mashabiki wa soka wakitarajia kuona ubora wa vikosi vya timu hizo mbili kubwa nchini kabla ya kuanza kwa kampeni za mashindano mengine.