Kundi la wanamgambo wa Palestina la Hamas limetangaza hii leo kumchagua mujahid Khalil al-Hayya kuwa kiongozi wake mkuu.
Afisa mmoja wa Hamas ameliambia shirika la habari la AFP Khalil al-Hayya alichaguliwa kwa idadi kubwa ya kura na kuongeza kuwa huenda akaanza majukumu yake rasmi wiki ijayo.
Anachukua nafasi ya kiongozi wa Hamas aliyeuawa Yahya al-Sinwar, ambaye Israel ilimshutumu kuwa miongoni wa waratibu wakuu wa mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 aliuliwa na vikosi vya Israel huko Gaza mwaka 2024.
Tangu kifo chake, Hamas wamekuwa wakiongozwa na baraza la wajumbe watano, lililosimiwa na afisa mwandamizi wa muda mrefu Mohammed Darwish.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime