Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema mashambulizi yamefanyika katika bandari za Odesa na Chornomorsk kwa kutumia makombora ya masafa marefu na droni.
Urusi imeendelea kushambulia usiku kucha miundombinu ya bandari nchini Ukraine, ikidai imelenga maeneo yaliyokuwa yakitumika kupeleka vifaa kwa jeshi la Ukraine pamoja na meli nne zilizokuwa zikisafirisha mizigo ya kijeshi.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema mashambulizi hayo yalifanyika katika bandari za Odesa na Chornomorsk kwa kutumia makombora ya masafa marefu na droni.
Kwa upande wake, maafisa wa Ukraine wamesema mashambulizi hayo yameharibu miundombinu ya kiraia, viwanda na bandari katika mikoa ya Odesa na Mykolaiv, huku mtu mmoja akijeruhiwa.Mapigano Bahari Nyeusi yazidi kuhatarisha biashara
Wakati huo huo, rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ambaye amewasili Kiev leo katika siku ya kumbukumbu ya kitaifa ya kuenzi kushamiri kwa tamaduni za Ukristo nchini Ukraine, pamoja na viongozi wengine wa mataifa ya Ulaya, ametangaza mipango mipya ya kijeshi kwa Ukraine.
Kadhalika rais wa Lithuania Gitanas Nauseda amesema nchi yake imeimarisha ulinzi wa miundombinu ya nishati na usafiri kutokana na taarifa za kijasusi zinazoashiria Urusi huenda ikapanga mashambulizi dhidi ya miundombinu hiyo.