Lebanon na Israel wamerejea kwenye mazungumzo hii leo mjini Rome, huku Beirut ikitarajia kutafikiwa hatua katika suala la Israel kuondoka kusini mwa Lebanon chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani.
Maafisa wa pande hizo mbili watakutana kwenye ubalozi wa Marekani mjini humo leo na kesho ili kuangazia namna ya kutekeleza makubaliano ya kimkakati, maafisa wa Lebanon wameiambia Reuters.
Rais wa Lebanon Joseph Aoun alisema jana Jumatatu kwamba anatarajia mkutano wa Roma utaibua "hatua za dhahiri, za vitendo na zenye uhalisia” za kutekeleza makubaliano hayo, yatakayoshuhudia Israel ikiondoa wanajeshi wake.
Jeshi la Israel linadhibiti eneo inaloliita "ukanda salama” wa takriban kilomita 10 ndani ya Lebanon linalopakana na mpaka wa Israel, kwa madai ya kulinda jamii za kaskazini mwa Israel dhidi ya mashambulizi ya Hezbollah.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime