Urusi yafanya mashambulizi mapya ya makombora dhidi ya Kiev

Urusi imefanya mashambulizi mapya ya usiku kucha ya makombora ya balistiki dhidi ya mji mkuu wa Ukraine Kiev huku milipuko kadhaa ikisikika katikati ya jiji. Haya yamesemwa leo na mamlaka nchini Ukraine.

Mamlaka mjini Kiev imesema moto ulizuka katika wilaya mbili, huku baadhi ya matukio hayo yakisababishwa na mabaki ya makombora yaliyoanguka.

Makombora ya balistiki ni magumu sana kuzuiwa kutokana na kasi yake kubwa.

Mashambulizi hayo yametokea muda mfupi baada ya baadhi ya wanachama wa kile kiitwacho "muungano wa walio tayari", unaojumuisha zaidi ya nchi 35 zinazoiunga mkono Ukraine katika kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi, kuzindua mpango mjini Paris nchini Ufaransa wa kuimarisha ulinzi wa anga wa Ukraine.

Ukraine imekuwa ikijitetea dhidi ya uvamizi kamili wa Urusi kwa zaidi ya miaka minne, kwa msaada wa mataifa ya Magharibi.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii