Iran imetangaza kuwa haitoendelea kuheshimu makubaliano ya usitishaji vita, iliotia saini na Marekani kama Washington haitotimiza ahadi yake ya kusitisha vita hivyo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Iran Esmaeil Baqaei amedai kuwa kila Mara Marekani iliposhindwa kuheshimu makubaliano hayo na Iran pia iliacha kuyatekeleza akisema hivyo ndio Iran itakavyoendesha suala hilo hadi pale Marekani itakapotimiza kikamilifu wajibu wake katika vita hivyo.
Marekani na Iran zimedai kudhibiti Mlango Bahari wa Hormuz, kufuatia mashambulizi mapya kati yao yaliyoanza upya wiki iliyopita, hali ambayo imezidi kutishia juhudi za kidiplomasia za kumaliza vita.
Madai hayo yanakuja wakati mvutano kati ya pande hizo mbili ukiendelea kuongezeka, huku mashambulizi ya hivi karibuni yakisababisha hofu kuhusu usalama wa njia hiyo muhimu ya bahari inayosafirisha asilimia 20 ya mafuta ya dunia.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime