Mlipuko wa Ebola unasambaa kwa kasi 'kutisha'

Mamlaka za Afya barani Afrika zimesema mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndio "unasambaa kwa kasi zaidi" kuwahi kushuhudiwa.

Mkuu wa Kitengo cha Dharura katika Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika, CDC, Wessam Mankoula amesema mlipuko huu ndio unaokua kwa kasi zaidi si tu ukilinganishwa na milipuko ya awali ya virusi vya Bundibugyo, bali pia ukilinganisha na aina zote za virusi vinavyosababisha Ebola.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa ni bahati mbaya kwamba virusi hivyo vya Ebola vinasambaa kwa kasi kuliko juhudi za kukabiliana navyo na kungeza kuwa idadi ya visa inakadiriwa kuongezeka mara mbili kila baada ya siku 28.

Amesema kunahitajika dola bilioni 1.4 kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo pamoja na mahitaji ya kibinadamu yanayotokana na mlipuko huo na kuwahimiza washirika kuongeza kasi ya mwitikio, akimaanisha rasilimali za kifedha na rasilimali watu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii