Klabu ya Azam FC leo Agosti 5, 2026, imezindua rasmi jezi zitakazotumika katika msimu wa mashindano wa 2026/27, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Kupitia kurasa zake rasmi za mtandao wa Instagram, klabu hiyo imewaonyesha mashabiki wake muonekano wa jezi hizo mpya kwa kuchapisha picha na video maalum za utambulisho.
Jezi hizo zinatarajiwa kutumika katika mashindano mbalimbali ambayo Azam FC itashiriki msimu ujao, ikiwemo Ligi Kuu ya NBC pamoja kuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Shirikisho la CAF.