Kura za maoni zinatabiri matokeo mabaya kwa chama chake cha Labour, ambapo ikiwa mambo yatakwenda kombo hali hiyo inaweza kuongeza shinikizo kwa Starmer.
Wapiga kura nchini Uingereza
wanapiga kura leo katika uchaguzi unaotarajiwa kuongeza
shinikizo zaidi kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Keir Starmer.
Wapiga kura wanaelekea kwenye sanduku la kura katika kile
kinachotajwa kuwa ni mtihani mkubwa kwa kiongozi huyo tangu ushindi wake mkubwa
katika uchaguzi mkuu wa Julai 2024 uliomaliza miaka 14 ya utawala wa chama cha
Conservative.
Kura za maoni zinatabiri matokeo mabaya kwa chama chake cha Labour ambapo ikiwa mambo yatakwenda
kombo hali hiyo inaweza kuongeza shinikizo kwa Starmer.
Umaarufu wa kiongozi huyo umepungua na kulingana na utafiti wa
maoni ya wapiga kura, Waingereza wengi wanamtaja kama Waziri mkuu aliyefanya
vibaya zaidi.
Uchaguzi huu pia unatajwa kuwa utaonyesha ongezeko kubwa la watu wenye kufuata sera za itikadi kali za mrengo wa kulia na kushoto.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime