Rais Trump akutana na mwenzake wa China Xi Jiping jijini Beijing

Rais wa Marekani Donald Trump, amepokea mapokezi makubwa jijini Beijing nchini China, mbele ya mwenyeji wake Xi Jinping wakati huu, wakianza mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kibiashara, vita vya Iran na hatua ya Marekani kuiuzia Taiwan silaha.

Rais Xi Jinping, amemwambia Donald Trump kuwa China na Marekani, zinapaswa kuwa washirika badala ya kuwa washindani hasa kwenye masuala ya biashara, ili ziwe thabiti zaidi.

“Nakupongeza wewe na watu wa Marekani, siku zote naamini kuwa maslahi yanayotuunganisha sisi China na Marekani, ni makubwa kuliko tofauti zetu. Mafanikio ya China na Marekan ni fursa kwa sisi sote.” Amesema Rais Xi.

Naye Trump, ambaye amerejea Beijing kwa mara ya kwanza kama rais wa Marekani tangu mwaka 2017, amemwambia mwenyeji wake kuwa nchi hizo zitakuwa na ushirikiano mzuri.

“Tutakuwa na siku nzuri za usoni pamoja, naheshimu sana China, wewe ni kiongozi imara, hili huwa nalisema kila wakati. Ni fahari sana kuwa hapa, na uhusiano kati ya Marekani na China, utaimarika zaidi.” Amesema Rais Trump.

Ziara hii imekuja wakati huu mataifa haya mawili yenye uchumi mkubwa duniani, yakiendelea kukabiliwa na mvutano wa kibiashara.

Wachambuzi wa mambo wanasema, rais Trump anatumia ziara hii kuona ni nini China inaweza kufanya kusaidia kumaliza vita nchini Iran.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii