Sudan Kusini inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu mwezi Desemba mwaka huu baada ya miaka mingi ya kucheleweshwa mara kwa mara.
Na itakumbukwa kuwa uchaguzi huo uliotakiwa
kufanyika tangu mwaka 2022 licha ya nchi hiyo kuwa
ukingoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na mivutano kati ya rais
Salva Kiir na Makamu wake Riek Mashar.
Ambapo hayo yamebainishwa na Waziri wa habari wa nchi hiyo Ateny Wek Ateny,
ambaye amesisitiza kuwa kwa sasa nchi hiyo inashuhudia hali ya utulivu ispokuwa
katika jimbo la mashariki mwa Jonglei.
Huu utakuwa uchaguzi wa kwanza tangu Sudan Kusini ipate uhuru kutoka kwa Sudan mnamo mwaka wa 2011.
Hata hivyo nchi hiyo masikini inazongwa na ufisadi uliokithiri, huku vifungu kadhaa vya makubaliano ya amani vikiwa havijafikiwa, ikiwa ni pamoja na kuunganisha vikosi vya kijeshi vinavyoendelea kupingana.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime