Watu 30 wauwawa katika mkanyagano Haiti

Takriban watu 30 wamekufa katika mkanyagano wa watu katika ngome ya kihistoria kaskazini mwa Haiti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa serikali ya Haiti, tukio hilo lilitokea jana Jumamosi katika Citadelle Laferrière huko Milot wakati wa "shughuli ya utalii iliyowakusanya vijana wengi.”

Jean Henry Petit, mkuu wa ofisi ya ulinzi wa raia kaskazini mwa Haiti, aliambia gazeti la ndani Le Nouvelliste kwamba angalau watu 30 waliuawa katika ngome hiyo ya karne ya 19 ambayo imetambuliwa kama moja ya Turathi za Dunia za UNESCO

Petit alisema idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoripotiwa kutojulikana waliko.

Kadhalika, watu kadhaa walijeruhiwa na kupelekwa hospitali, ingawa idadi kamili haikutolewa. Ripoti za awali zilisema kuwa wageni walikuwa wamebanwa katika lango moja la kuingilia, na vurugu zilianza kati ya watu waliokuwa wakijaribu kutoka na wale waliokuwa wakiingia.

Serikali imewahimiza wananchi "kuwa watulivu na waangalifu” wakati uchunguzi ukiendelea.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii