April 7, 1994 ni siku ya ambayo historia ya Rwanda ilianadikwa kwa wino mwekundu kumaanisha hatari, kifo cha Rais zamani wa Taifa hilo Juvenal Habyarimana aliuawa akitokea nchini Tanzania katika mchakato wa kusaka amani nchini Rwanda, baada ya waasi wa kundi la RPF wakati huo, ambalo kwa sasa ni chama kilichopo madarakani, kuanzisha vita dhidi ya serikali ya Juvenal Habyarimana, wakimtuhumu kuwatenga raia wa Rwanda kutoka jamii ya watutsi.
Hapo ndipo ghasia zikazuka kote nchini humo kwa jamii ya Wahutu na Watutsi kushambuliana vikali kutoka mijini hadi katika vijiji.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime