Bodi ya Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) imemteua rasmi Rais wa Klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said, kuwa balozi wa Kiswahili ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa BAKITA, Bi. Consolata Mushi, uteuzi huo unamfanya Hersi Said kuwa miongoni mwa mabalozi watatu wa Kiswahili walioteuliwa na taasisi hiyo.
Hata hivyo mabalozi wengine waliotajwa ni Mama Salma Kikwete pamoja na Jorum Mkumbi BAKITA imeeleza kuwa uteuzi huo unalenga kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili kimataifa, hasa kutokana na mchango wa lugha hiyo katika utambulisho wa Tanzania na Afrika Mashariki.
Bi. Consolata Mushi amesisitiza kuwa mabalozi hao watasaidia kuimarisha hadhi ya Kiswahili ndani na nje ya nchi kupitia majukwaa yao mbalimbali ya kijamii, kisiasa na michezo.
Hatua hiyo inaendelea kuonyesha juhudi za Tanzania katika kukuza Kiswahili kama lugha ya kimataifa, huku ikipata nguvu kupitia viongozi na watu mashuhuri wenye ushawishi katika jamii.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime