Iran na Marekani kufanya mazungumzo nchini Pakistan

Pakistan inajiandaa Ijumaa kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani kati ya Marekani na Iran kujaribu kutuliza mvutano na kuokoa makubaliano ya usitishwaji mapigano kwa muda wa wiki mbili ambayo yako hatarini kuvunjika.

Kuwait imeilaumu Iran kwa mashambulizi ya droni huku rais wa Marekani Donald Trump akionyesha mashaka kuhusu makubaliano hayo hasa kutokana na Iran kuendelea kuwa na udhibiti kamili wa Mlango-Bahari wa Hormuz, miongoni mwa mada itakayojadiliwa huko Islamaba.

Wakati huohuo, Israel na Lebanon zinatarajiwa pia kufanya mazungumzo mjini Washington wiki ijayo huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akishinikiza kupokonywa silaha kwa wanamgambo wa Hezbollah.

Lakini afisa mmoja wa serikali ya Beirut amesema wanahitaji kwanza makubaliano ya kusitisha mapigano kabla ya kuanza mazungumzo yoyote na Israel.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii