Benki ya Dunia: Ukuaji wa uchumi kupungua Afrika

Ripoti ya Benki ya Dunia imesema ukuaji wa uchumi katika mataifa ya Afrika yaliyopo Kusini mwa Jangwa la Sahara utapungua kutoka asilimia 4.4 hadi 4.1 mnamo mwaka huu 2026 kutokana na vita vya Mashariki ya Kati.

Ingawa ripoti hiyo iliyotolewa wiki hii na Benki ya Dunia imesema kutashuhudiwa tatizo katika uagizaji wa bidhaa muhimu kama mafuta na mbolea huku nchi zenye matatizo ya kiuchumi na kifedha  kama Burundi, Malawi, Ethiopia, Kenya na Msumbiji zikiathirika pakubwa.

Hata hivyo kumekuwa pia na wasiwasi kuhusu uwekezaji wa mataifa ya Ghuba barani humo, ambayo yamekuwa wawekezaji wakubwa hasa Afrika Mashariki, katika sekta mbalimbali ikiwemo madini, nishati mbadala na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA)

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii