BUNGE Spika wa Bunge la Tanzania Mussa Azzan Zungu ameeleza utaratibu wa Bunge katika kushughulikia Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambapo amebainisha kuwa kamati za kusimamia fedha za umma zinapaswa kuanza kazi mara moja pindi ripoti hizo zitakapoanza kujadiliwa ndani ya Bunge la Tanzania.
Akiwa Bungeni leo Aprili 10, 2026, Spika ameweka bayana kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha uwajibikaji na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma mara tu taarifa za CAG zinapowasilishwa.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime