Viongozi wa Dini wa Madhehebu mbalimbali Nchini wamekumbushwa kuimarishwa Mahusiano kati ya Taasisi za Dini na Serikali ili kudumisha Amani Umoja na Mshikamano huku Vijana iwakikumbushwa kutumia fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi
Ujumbe huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Deus Sangu wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Shekina Jijini Dar es Salaam
Vilevile Mchungaji wa Kanisa la Shekina, Daniel Mulesi, ametambulisha rasmi Shekina Shop application mpya huku lengo kuu la application hiyo ni kurahisisha biashara kwa kuwapa fursa watu wasiokuwa na mtaji kuuza bidhaa zao kwa urahisi zaidi, pamoja na kuchangia kuongeza ajira kwa Watanzania kupitia mfumo wa kidigitali.
Hatua hii inatajwa kuwa sehemu ya juhudi za kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika sekta ya biashara nchini.