Karibu watu 70 wamekamatwa na mamlaka ya Iran, wakituhumiwa kwa kuhusishwa na mitandao ya ujasusi ya kigeni katika jimbo la Mazandaran, kulingana na shirika la habari la Tasnim.
Idara za ujasusi ziliwatambua washukiwa wakati wa operesheni zilizofanywa kote katika jimbo hilo na kuwashutumu kwa kukusanya taarifa kwenye tovuti nyeti na kufanya hujuma.
Shirika la habari la Iran pia limeripoti kwamba mamlaka zilikamata silaha za moto, silaha za jadi, na vifaa vya mawasiliano wakati watu hao walipokamatwa. Mbali na hayo, wamesema kwamba walikamata mitambo ambayo hutumika kwa kutumia intaneti kwa setilaiti inayodaiwa kutumika kusambaza data kwa idara za ujasusi za kigeni.
Vikosi vya usalama vya Iran vimesema kwamba kundi hilo liliendelea kuwasiliana na maadui wakati wa vita vya siku 12 mnamo mwezi Juni 2025 na kwamba wanachama wake waliendelea kushiriki taarifa hadi walipokamatwa.