Mazungumzo ya amani kati ya Iran na Marekani "yamepiga hatua," lakini makubaliano ya mwisho "bado yako mbali," spika mwenye wa bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema siku ya Jumamosi, Aprili 18.
"Bado tuko mbali na kukamilisha majadiliano," Ghalibaf, ambaye alishiriki katika mazungumzo na Marekani wiki iliyopita huko Islamabad, aliiambia televisheni ya Iran katika mahojiano.
"Tumepiga hatua katika mazungumzo, lakini tofauti nyingi bado zipo, na baadhi ya mambo ya msingi bado hayajatatuliwa," aliongeza.
Wakfu wa Mashahidi nchini Iran uliripoti siku ya Jumamosi kwamba watu 3,468 wameuawa katika vita vkati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran kwa karibu wiki sita. "Faili imefunguliwa kwa ajili ya mashahidi 3,468 waliouawa wakati wa mzozo wa hivi karibuni," alisema Ahmad Mousavi, mkuu wa Wakfu wa Mashahidi, akinukuliwa na shirika la habari la ISNA.
Idadi ya awali iliyotolewa Aprili 12 na Shirika la Tiba la Iran iliripoti vifo 3,375. Shirika lisilo la kiserikali la Haki za Binadamu, Human Rights Activists News Agency (HRANA) lenye makao yake nchini Marekani, lilihesabu vifo vya angalau watu 3,636, ikiwa ni pamoja na raia 1,701—miongoni mwao watoto angalau 254—wanajeshi 1,221, na watu 714 ambao hali yao haikutajwa.