Ujerumani yatoa msaada wa euro milioni 20 kwa Sudan

Ujerumani iimesema itatoa euro milioni 20 zaidi kwa Sudan mwaka huu, huku ahadi zaidi za ufadhili zikipitiwa upya msaada huo unatolewa huku mzozo wa Sudan ukiingia mwaka wake wa nne Jumatano.

Ujerumani itatoa euro milioni 20 zaidi kwa Sudan mwaka huu, huku ahadi zaidi za ufadhili zikipitiwa upya kwa sasa.

Hayo yamesemwa leo na wizara ya maendeleo ya Ujerumani mjini Berlin katika taarifa, huku wafadhili wa kimataifa wakikusanyika kwa mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu Sudan ikiwa imetimia miaka mitatu kamili tangu kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Mwishoni mwa mwaka wa 2025, wizara hiyo ilikuwa imetoa euro milioni 155.4 kwa miradi nchini Sudan na katika nchi jirani zilizoathiriwa na vita nchini Sudan, ambazo ingeongeza mwaka huu kwa euro milioni 20.

Kabla ya mkutano Berlin shirika la misaada la Save the Children tawi la Ujerumani limetoa wito kufanyike juhudi kubwa zaidi za kuwalinda raia Sudan.

Afisa Mkuu mtendaji wa shirika hilo Florian Westphal ametoa wito hatua zichukuliwe kukabiliana kikamilifu na mgogoro wa Sudan na kutaka mkutano wa Berlin ulete tija katika kuutafutua ufumbuzi mzozo huo.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii