Zelensky asema Marekani haina muda na vita vya Ukraine

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema vita vya Iran vimesababisha mkwamo katika juhudi za kuvimaliza vita vinavyoendelea nchini mwake dhidi ya Urusi na hata kutatiza msaada wa silaha kutoka Marekani.

Zelensky ameliambia shirika la utangazaji la Ujerumani, ZDF kwamba hivi sasa wapatanishi wa ngazi ya juu wa Marekani "hawana muda kwa ajili ya mzozo wa Ukraine" na wamewekeza nguvu katika kushughulikia vita vya Iran.

Amesema wajumbe wa Rais Donald Trump ambao ni Steve Witkoff na Jared Kushner, waliokuwa na jukumu la kuratibu mazungumzo na Urusi ili kuvimaliza vita vya Ukraine, hivi sasa wanaongoza majadiliano kati ya Marekani na Iran.

Kwenye mahojiano hayo na ZDF, kiongozi huyo wa Ukraine, ameelezea wasiwasi kwamba iwapo Marekani haitoongeza shinikizo kwa Rais Vladimir Putin vita vinavyoendelea havitafikia mwisho.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii