Papa azuru mji wa Cameroon kwa awamu ya pili ya ziara yake Afrika.

Kiongozi wa kanisa Katoli duniani Papa Leo XIV anatarajiwa kuwasili nchini Cameroon Jumatano. Akiwa nchini humo atakutana na rais Paul Biya mjini Yaoundé.

Kiongozi wa kanisa Katoli duniani Papa Leo XIV anatarajiwa kuwasili Cameroon leo Jumatano ambako atakutana na rais wa nchi hiyo Paul Biya mjini Yaoundé katika awamu ya pili ya ziara yake barani Afrika.

Biya, mwenye umri wa miaka 93, amekuwa rais wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi tangu 1982 na aliwahi kuwa waziri mkuu kabla ya hapo.

Zaidi ya nusu ya wakazi milioni 30 wa Cameroon ni wakristo, huku robo kati yao wakiwa Wakatoliki, kulingana na hifadhi ya data za kidini ya dunia.

Papa anakwenda Cameroon baada ya kukosolewa upya na rais wa Marekani Donald Trump kuhusu miito yake ya kuifikisha mwisho mizozo ya dunia, akituhumiwa kwa kupuuza ukandamizaji wa iran dhidi ya waandamanaji mapema mwaka huu.

Hata hivyo Papa Leo anawasili Camroon akitokea Algeria, kituo chake cha kwanza cha ziara yake ya Afrika itakayompeleka pia nchini Angola na Guinea ya Ikweta.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii