Waingereza wakamatwa UAE Kwa kupiga picha mashambulizi ya Makombora

Waingereza watano wanashikiliwa na mamlaka za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), huku wengine zaidi ya 70 wakidaiwa kukumbwa na mkono wa sheria tangu kuanza kwa mashambulizi yanayohusishwa na Iran mwishoni mwa Februari.

Kukamatwa huko kunahusishwa na mvutano unaoendelea Mashariki ya Kati baada ya Iran kuanza mashambulizi dhidi ya maeneo ya UAE mwishoni mwa mwezi Februari katika miji kama Dubai watalii na wakaazi walionekana kurekodi matukio hayo bila kufahamu athari za kisheria.

Mamlaka za UAE zimeimarisha utekelezaji wa sheria za mtandao na usalama wa taifa, zikionya kuwa kupiga au kusambaza picha za matukio ya kijeshi ni kosa kubwa la jinai.

Sasa, hata kuwa na picha hizo kwenye simu bila kuzisambaza kunaweza kusababisha kukamatwa. Adhabu inaweza kufikia kifungo cha hadi miaka 10 jela au faini ya hadi pauni 200,000.

Kundi la kampeni la Dubai Watch linadai zaidi ya Waingereza 70 wamekamatwa tangu kuanza kwa vita ambapo mwanzilishi wake, David Haigh, amesema takribani watu 35 wanashikiliwa Dubai na wengine karibu idadi hiyo katika Abu Dhabi.

Baadhi ya waliokamatwa, wakiwemo wafanyakazi wa ndege, wanaripotiwa kushikiliwa katika vituo vilivyojaa watu wengi na wakati mwingine kunyimwa usingizi, chakula na hata huduma za matibabu.

Haigh amesema hali imezidi kuwa mbaya:

“Awali walikuwa wanatoa tu onyo mtandaoni, lakini sasa wanakamata watu na kuwapeleka jela.”

Ameongeza kuwa polisi sasa wanakagua simu za watu katika maeneo ya tukio, na hata kupokea au kuhifadhi picha kunaweza kuchukuliwa kama kosa.

Katika kesi zinazotia wasiwasi Kuna tukio la mtalii wa Uingereza mwenye umri wa miaka 60 aliyekamatwa baada ya kudaiwa kurekodi makombora karibu na Jebel Ali Port ingawa alifuta video hiyo mara moja, bado alishtakiwa pamoja na watu wengine 20 chini ya sheria za mtandao za UAE.

 Hata hivyo kwa mujibu wa Radha Stirling wa Detained in Dubai, sheria hizo ni pana na zinaweza kuwahusisha hata watu wanaoshiriki au kutoa maoni kwenye video zilizopo mtandaoni.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii