Asilimia 51 ya Gen Z Wadai Degree Ni Hasara

Kwa mujibu wa takwimu mpya kutoka Indeed Survey, asilimia 51 ya vijana wa kizazi cha Gen Z wenye shahada wanasema elimu yao ni upotevu wa pesa, wakilalamikia gharama kubwa za masomo na madeni yanayowakwamisha kiuchumi.

Takribani asilimia 38 wanaeleza kuwa madeni ya chuo yanazuia maendeleo yao ya kazi, huku mabadiliko ya soko la ajira—ikiwemo kuongezeka kwa matumizi ya AI na kupewa kipaumbele kwa ujuzi na uzoefu—yakiwafanya baadhi ya waajiri kupunguza thamani ya degree, jambo linalosababisha wengi kufanya kazi zisizoendana na taaluma walizosoma.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii