Mwanamuziki wa zamani wa Hip Hop aliyegeukia siasa Balen Shah, ameapishwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Nepal kufuatia ushindi mkubwa wa chama chake katika uchaguzi wa bunge.
Shah, mwenye umri wa miaka 35 na aliyewahi kuwa meya wa Kathmandu, anaingia madarakani akiwa mmoja wa viongozi vijana zaidi kushika wadhifa huo na wa kwanza kutoka jamii ya Madhesi.
Aidha chama chake cha Rastriya Swatantra Party kilipata ushindi wa viti 182 kati ya 275, na baada ya kuapishwa ametangaza baraza dogo la mawaziri lenye wajumbe 14 ili kupunguza matumizi ya serikali.
Hata hivyo pamoja na ushindi huo bado anakabiliwa na changamoto ya kurejesha utulivu wa kisiasa na kushughulikia athari za maandamano ya mwaka 2025 yaliyosababisha vifo vya watu 76 chini humo.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime