Cuba yaanza kuwaachia maelfu ya wafungwa

Mamlaka za Cuba zimeanza kuwaachilia wafungwa baada ya kutangaza kuwa nchi hiyo itatoa msamaha kwa wafungwa 2,010. Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha chini ya mwezi mmoja.


Zaidi ya wafungwa 20 waliachiliwa kutoka gereza la La Lima mashariki mwa Havana, wakiwa wameshikilia nyaraka zao za kuwa huru, wakilia na kuwakumbatia jamaa zao ambao walikuwa wakiwasubiri tangu asubuhi.

Hata hivyo hadi sasa haijajulikana kama wale walioachiliwa Ijumaa ni wafungwa wa kisiasa, kwani hakuna orodha iliyochapishwa. Mamlaka za Cuba zinakana kuwashikilia wafungwa wa aina hiyo.

Aidha wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema inafahamu taarifa kuhusu kuachiliwa kwa wafungwa, lakini ikaongeza kuwa haijulikani wazi kama wafungwa wowote wa kisiasa watakuwa miongoni mwao.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii