Zelenskiy Atoa Ofa ya Ulinzi wa Bahari kwa Strait of Hormuz

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, ametangaza kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na mataifa ya Mashariki ya Kati katika kulinda usalama wa usafiri wa baharini kwenye eneo nyeti la Strait of Hormuz, huku mvutano wa kijeshi ukiendelea katika ukanda huo.

Akizungumza kupitia hotuba yake ya kila usiku, Zelenskiy alisema Ukraine ina uzoefu mkubwa katika kulinda njia za majini na kuhakikisha uhuru wa meli kupita salama, uzoefu uliopatikana wakati wa vita dhidi ya Urusi katika Bahari ya Black Sea.

“Ukraine ina utaalamu wa kipekee katika ulinzi na ufunguaji wa njia za usafiri wa baharini. Tuko tayari kushirikiana na washirika wetu ili kuimarisha usalama,” alisema.

Tamko hilo linakuja baada ya mkutano wa mtandaoni uliowakutanisha takriban nchi 40 kujadili namna ya kuhakikisha njia ya Hormuz inabaki wazi, hasa wakati huu ambapo kuna mvutano mkubwa wa kijeshi unaohusisha mataifa ya Mashariki ya Kati.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha, alihudhuria mkutano huo kwa niaba ya nchi hiyo.

Teknolojia ya kivita ya Ukraine
Katika miaka minne ya vita, Ukraine imefanikiwa kuendeleza teknolojia za kisasa za kijeshi, ikiwemo drone za baharini ambazo zimeisaidia kufanya mashambulizi dhidi ya meli za Urusi na kuzuia udhibiti wa Bahari ya Black Sea.

Teknolojia hiyo sasa inaonekana kuvutia mataifa mengine yanayotafuta njia za kulinda miundombinu yao ya baharini na njia muhimu za biashara.

Zelenskiy pia alifichua kuwa tayari Ukraine ina ushirikiano na nchi kadhaa za Mashariki ya Kati ikiwemo Saudi Arabia, United Arab Emirates, Qatar na Jordan.

Aidha, mazungumzo yanaendelea na mataifa mengine kama Bahrain, Kuwait, Iraq pamoja na Turkey ili kufanikisha mikataba ya usalama na teknolojia.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii