Watoto wanne wameuawa kwa kuchomwa kisu shuleni nchini Uganda

Nchini Uganda, watoto wanne wamechomwa kisu hadi kufa katika shule moja ya chekechea katika mtaa wa Ggaba nje kidogo ya jijiji kuu Kampala.

Polisi wamesema mtuhumiwa wa shambulio hilo Christopher Okello Onyu, mwenye umri wa miaka 34, alijifanya mzazi kabla ya kuanza kutekeleza uhalifu huo.

"Mshukiwa anadaiwa kuja hapa siku chache zilizopita akitafuta nafasi kwenye shule hii na akaambiwa arejea tena  na akafanya n ahata kulipa karo ambapo baada ya kufanya hivyo alienda kuwashambulia watoto ambao walikuwa wakicheza kwenye uwanja wa shule na kuwauwa wanne kwa kuwachoma kisu.  Watoto waliouwa watatu ni wa kiume na mmoja ni wa kike. Watoto watatu walifariki wakati wakipelekwa hospitalini wakati mwengine akifariki kwenye eneo la tukio." Alisema  Rachael Kawala, Msemaji wa Polisi Uganda.

Mshukiwa alikamatwa kwenye eneo la tukio na anazuiliwa na maofisa wa polisi kwa mujibu wa mamlaka. Sababu ya yeye kuteleza shambulio hilo bado haijabainika.

Milly Nassozi ni mkaazi wa eneo la Ggaba Kampala.

"Nilikuwa kwenye saloon yangu na mteja, na tulikisika kelele ambapo tuliona wahudumu wa bodaboda wakielekea huko shuleni. Tuliwafuata kule walikokuwa wakienda na kisha tukapata watoto wakiwa wameuwa na mshukiwa alikuwa akitoroka kabla ya kukamatwa na kurejeshwa ndani." Alisema  Milly Nassozi ni mkaazi wa eneo la Ggaba Kampala.

Aidha ametoa wito wa serikali ya Uganda kuimarisha usalama wa wanafunzi wakiwa shuleni.

"Tunatoa wito kwa serikali kuimarisha usalama wa wanafunzi shuleni. Wale ni watoto wadogo sana wanaoenda hapo shuleni. Eneo hilo linahitaji usalama wa kutosha." Alisisitiza  Milly Nassozi ni mkaazi wa eneo la Ggaba Kampala.

Mashambulio dhidi ya wanafunzi shuleni sio kawaida nchini Uganda, tukio hili la wiki hii likiibua hitaji la kuimarishwa kwa usalama zaidi katika taasisi za elimu zikiwemo zile zinazotoa elimu kwa watoto wadogo.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii