Mwili wa Kardinali Pengo Waagwa Dar es Salaam

Mwili wa Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (81), unaagwa leo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu jijini Dar es Salaam, kufuatia kifo chake kilichotokea Februari 19, 2026 akiwa anapatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amesema waumini watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana, kabla ya misa takatifu itakayofanyika baadaye. Amesema ibada ya jioni pia itafanyika na mwili utalala kanisani hapo, huku waumini wakiruhusiwa kukesha kwa sala.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Ruwa’ichi, kesho mwili utapelekwa Kituo cha Hija Pugu kwa misa ya mazishi itakayoanza saa nne asubuhi, kisha kuzikwa katika kanisa hilo kwenye kaburi aliloliandaa mwenyewe Kardinali Pengo.

Hata hivyo ameongeza kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na aliwekewa kifaa maalum cha kusaidia mapigo ya moyo kufanya kazi kwa utaratibu unaotakiwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii