Mareani imesema itafuta hadhi ya ulinzi wa muda kwa baadhi ya wahamiaji kutoka Somalia ambapo hatua hii ni katika kuendeleza juhudi za rais Donald Trump kuwafukuza watu wengi kutoka nchini Marekani.
Utawala wa rais Donald Trump umesema utakomesha hadhi ya ulinzi wa muda kwa wahamiaji kutoka Somalia hatua ya hivi karibuni katika ajenda ya rais ya kuwafukuza watu wengi kutoka Marekani.
Hatua hiyo iliyotangazwa jana Jumanne inawaathiri mamia ya watu ambao ni kundi dogo la wahamiaji wanaoishi Marekani wakiwa na ulinzi wa muda.
Inakuja wakati wa msako wa uhamiaji wa Trump huko Minneapolis ambako Wasomali wengi wenyeji wanaishi na ambako maandamano ya mitaani yameongezeka tangu wakala wa uhamiaji na utekelezaji wa forodha wa Marekani alipomuua raia wa Marekani aliyekuwa akiandamana kupinga uwepo wa maafisa wa serikali ya shirikisho jijini humo.
Wizara ya usalama wa ndani ilisema katika taarifa kwamba Wasomali walioathiriwa lazima waondoke Marekani ifikapo Machi 17 wakati hadhi iliyopo ya ulinzi iliyorefushwa mara ya mwisho na rais wa wakati huo Joe Biden itakapofika mwisho.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime