Mamlaka za mahakama zimefungua uchunguzi na kutoa wito kwa mashahidi wowote kujitokeza kutoa taarifa kuhusu waziri wa zamani wa Burkina Faso, Yolande Viviane Compaoré aliyeuawa katika makazi yake mjini Ouagadougou.
Ambapo Maafisa wamesema kuwa mwili wa Compaoré uligunduliwa nyumbani kwake siku ya Jumamosi iliyopita, na ushahidi uliopatikana eneo la tukio unaonyesha kuwa alishambuliwa kisha kuuawa hivyo mamlaka za mahakama zimefungua uchunguzi na kutoa wito kwa mashahidi waliotazama tukio hilo kujitokeza kutoa taarifa.
Itakumbukwa kuwa Compaoré alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa wakati wa urais wa Blaise Compaoré. Aliwahi kuwa gavana wa Mkoa wa Kaskazini na mbunge wa chama tawala cha zamani, CDP, na alishika nyadhifa kadhaa za uwaziri, zikiwemo Waziri wa Uchukuzi na Utalii. Pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ulinzi hivyo serikali ya Blaise Compaoré iliondolewa madarakani kupitia uasi wa wananchi mwaka 2014, na rais huyo wa zamani kukimbilia Côte d’Ivoire.
Hata hivyo baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais Blaise Compaoré mwaka 2014, Rais wa Bunge Isaac Zida alichukua uongozi wa mpito, kisha nchi ikaongozwa na Rais wa mpito Michel Kafando hadi uchaguzi wa 2015 uliomleta madarakani Roch Marc Christian Kaboré; hata hivyo, Kaboré aliondolewa kwa mapinduzi ya kijeshi Januari 2022 na nafasi yake ikachukuliwa na Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, ambaye naye alipinduliwa Septemba 2022 na Kapteni Ibrahim Traoré, ambaye bado anaiongoza Burkina Faso hadi sasa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime