Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema baada ya karibu miaka minne ya vita, hali ya ugumu wa maisha nchini mwake inaendelea kuwa mbaya zaidi katika eneo la vita na kwa watu kote katika nchi hiyo huku kukiwa na baridi kali na hali ya joto chini ya sifuri kutokana na kuharibiwa kwa miundombinu iliyosababishwa na mashambulizi ya Urusi.
Akizungumza jana katika hotuba yake ya kila siku kwa njia ya video Zelensky alisema Ukraine imeshambuliwa tena na mashambulizi ya Urusi, na makombora 18 ya masara marefu, na kwamba ndege zisizo na rubani za kivita na makombora ya masafa ya kati pia yametumika.
Ndege zisizo na rubani za Urusi zilishambulia miundombinu katika mji wa Kryvyi Rih katikati mwa Ukraine leo Jumatano, na kulazimisha kukatika kwa umeme kwa dharura kwa zaidi ya wateja 45,000 na kuvuruga usambazaji wa joto.
Zelensky alisema mafundi umeme wamekuwa wakifanya kazi kwa wiki kadhaa kuhakikisha gridi ya umeme inafanya kazi, akiongeza kuwa baridi kali imeleta changamoto za ajabu.
Zelensky pia alisema mambo ni magumu kila mahali hivi sasa, lakini katika eneo la vita, hali ni ngumu zaidi na Ukraine inaendelea kuilinda ardhi yake.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime