Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Eng. Chacha Wambura amesema mafunzo ya madiwani wa Mkoa wa Geita ni muhimu katika kuwawezesha viongozi kushirikiana vyema na serikali na halmashauri ili kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi.
Amesema semina hiyo iliyoandaliwa na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo imekuja kwa wakati muafaka, akisisitiza kuwa baada ya mafunzo hayo viongozi wako tayari kuanza utekelezaji wa majukumu ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Hata hivyo Wambura ameongeza kuwa baada ya mafunzo, madiwani na viongozi wamejipanga kuanza mara moja mchakamchaka wa kusukuma mbele agenda ya maendeleo katika Mkoa wa Geita.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime