Nuhu aliyedai mwisho wa Dunia desemba 25 akamatwa

Nabli wa Ghana Nuhu Ebo anadaiwa kukamatwa kwa kosa la kuzua taharuki kwa kusambaza habari kuwa Mungu amemfunulia maono kwamba ataiagamiza Dunia kwa maji tena ifikapo Desemba 25 mwaka huu.

Aidha Nuhu tayari amejenga zaidi ya Safina 8 za kuwahifadhi watu ambao Mungu atakuwa amewachagua kuingia humo, amekuwa
akipokea michango kutoka kwa watu mbalimbali Duniani kote ili afanikishe ujenzi wa safina zake.

Hata hivyo Kufuatia hali hiyo tayari kuna watu wameweka imani kwake na kutoka nchi za mbali na karibu tayari wakijianda kuingia kwenye
safina zake kabla ya tarehe 25.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii