Naibu Waziri akagua karakana ya kisasa ya bidhaa za ngozi DIT Mwanza

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Wanu Hafidh Ameir amekagua karakana ya kufundishia na kujifunzia iliyojengwa katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Mwanza ambayo imewekewa vifaa vya kisasa kwa ajili ya mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi. 

Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi Bilioni 1.1 na vimenunuliwa na Serikali kupitia Mradi wa EASTRIP ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha mazingira ya utoaji wa mafunzo ya ufundi na kuongeza ujuzi wa vijana katika teknolojia ya ngozi.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii