UN yaomba ufadhili wa dharura kuhudumia wakimbizi Burundi

Umoja wa Mataifa umeomba ufadhili wa dharura kusaidia zaidi ya raia 80,000 waliokimbilia Burundi kufuatia mmapigano ya hivi karibuni yaliyotokea Kivu Kusini, hususani katika mji wa Uvira ambako kumeshuhudiwa wimbi jipya la wakimbizi tangu Disemba 5 mwaka huu wanaokadiriwa kufikia 80,000 wanaokimbilia nchini Burundi.

Aidha Wakimbizi hao wanajumuisha Wakongomani 71,989 na Waburundi 8,000 ambapo Shirika hilo ambalo linatarajia kupokea jumla ya wakimbizi wapya 90,000, limezindua kampeni ya msaada wa dola milioni 33 ili kuwahudumia wakimbizi na kuwapatia makaazi salama.

Hata hivyo Meya wa mji wa Rumonge kusini-magharibi mwa Burundi, Augustin Minani aliviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa hali ni mbaya mno katika mji huo ambapo wakimbizi kati ya 20,000 hadi 25,000 kutoka Kongo wamewasili na wanakosa mahitaji ya msingi ikiwemo chakula.ashambulizi mapya yaliyofanywa na kundi la waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii