Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia Watuhumiwa wanne (04) kwa tuhuma za kupatikana na meno ya tembo.
Mnamo novemba 26 mwaka huu katika kizuizi cha Polisi kilichopo kitongoji cha Kyamnyorwa Kata ya Kasharunga tarafa ya Kimwani Wilaya ya Muleba Mkoaani Kagera walikamata watuhumiwa wanne wakiwa na meno mawili ya tembo wakitokea kijiji cha Nyaishozi Wilaya ya Karagwe kupitia ziwa Burigi kwa njia ya Mtumbwi na kupokelewa na gari aina ya Toyota Corona rangi ya kijivu lenye usajiri namba T 181 DHR.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Blasius Chatanda amewataka wananchi wote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera limetoa onyo kali kwa wale wote waliyojihusisha na kitendo hicho na linaendelea na msako mkali ili kubaini mtandao mzima.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime