Mahakama ya Wilaya Temeke Jijini Dar es Salaam imemukumu kutumikia kifungo cha miaka 20 jela Rashidi Ruambo mwenye umri wa miaka 56 fundi ushonaji mkazi wa Yombo Makangarawe kwa kupatikana na hatia ya kosa la Shambulio la aibu
Hukumu hiyo imeitolewa Novemba 25 mqaka huu na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Temeke Mh. Janeth Kaluyenda akisoma hukumu hiyo amesema kuwa Mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo ambao pasi na chembe ya shaka umemtia hatiani mtuhumiwa huyo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa mnamo mwezi Novemba 24,2024 majira ya saa 06:00 mchana huko maeneo ya Yombo Makangarawe mtuhumiwa akiwa katika duka lake la ushonaji alimuita mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 6 mwanafunzi wa chekechea na kuanza kumchezea kwa kumuingizia vidole sehemu zake za uke na kisha mtoto huyo akaenda kumueleza mama yake juu ya kitendo hicho alichofanyiwa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime