Wafanyabiashara wa madini nchini wameendelea kuwasilisha madini mbalimbali katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kama sehemu ya maandalizi ya kuelekea mnada wa tatu wa madini ya vito unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha mnamo Alhamisi, Novemba 27 mwaka huu.
Aidha hatua hii inalenga kuhakikisha madini yote yanayokusudiwa kuuzwa yanachambuliwa na kuthaminishwa kabla ya kuingizwa kwenye mnada, hatua inayoongeza uwazi na kuimarisha thamani ya madini nchini.
Hata hivyo Mnada huo unatarajiwa kuvutia wanunuzi wa ndani, hivyo kuongeza fursa na ushindani kwa wafanyabiashara hivyo kuongeza ukuaji wa sekta ya madini.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime