Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Taasisi zake imeanza kufanya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Wizara wa mwaka 2021/22-2025/26.
Akifungua kikao hicho leo Novemba 25, mwaka huu jijini Dodoma, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndg. Methusela Ntonda alisema kuwa, Wizara inatekeleza Mpango Mkakati wa mwaka 2021/22-2025/26 ambapo zoezi hilo lilitanguliwa na Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango huo.
Alisema kuwa, kikao hicho ni Utekelezaji wa maelekezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu uliyoyatoa awali kwa Wizara na Taasisi za Umma.
Mchakato huo ni matokeo ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa wizara, kupitia utekelezaji wa mipango na bajeti ya kila mwaka ili kupima matokeo katika mpango mkakati unaoisha muda wake.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime