Ukraine yashinikiza kuwa na jeshi imara la askari 800,000

Ukraine inasisitiza kuwa na nguvu ya askari 800,000 katika jeshi lake chini ya pendekezo lililoboreshwa la mpango wa amani lililowasilishwa kwa Marekani Volodymyr Zelensky amesema kuwa rasimu ya sasa yenye vipengele 20 imefanyiwa marekebisho ya kutosha.

Aidha katika Mpango wa awali wa Marekani uliowekwa wazi mwezi Novemba uliipangia Ukraine kikomo cha askari 600,000.

Hata hivyo wachambuzi wameonyesha mashaka kuhusu uwezo wa Ukraine kufikia idadi hiyo. Kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashtaka, kumekuwa na zaidi ya matukio 300,000 ya askari kutoroka au kutohudhuria kazini tangu uvamizi wa Urusi.

Hivyo kabla ya vita hiyo kuanza Ukraine ilikuwa na jeshi la kudumu lenye takriban askari 290,000 ili kufidia upungufu wowote wa wanajeshi, Kyiv inatarajia washirika wake wa Magharibi kuchangia kuongeza nguvu ya kijeshi endapo makubaliano ya amani yatafikiwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii