Wananchi wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kuendelea kulinda amani na usalama katika maeneo yao ili kuimarisha maendeleo ya taifa.
Wito huo umetolewa leo Novemba 24 mwaka huu kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Tanga, ACP NG’EVE, ambaye aliongozana na mwandishi mkongwe, mdau wa amani na maendeleo kutoka Tanga, Hassan Hashim, kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma.
ACP NG’EVE amesisitiza ushirikiano kati ya wananchi na Jeshi la Polisi pamoja na umuhimu wa kutoa taarifa mapema za viashiria vya uhalifu na kulinda miundombinu ya taifa.
Kwa upande wake, Hassan Hashim ameeleza kuwa amani huongeza uwekezaji, utalii na umoja wa wananchi, huku kukosekana kwake kukisababisha kudorora kwa shughuli za maendeleo.
Amehimiza matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, akiwataka vijana na wananchi kwa ujumla kujiepusha na uchochezi wa mitandaoni, na kusisitiza umuhimu wa kudumisha amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime