Katika kukabiliana na wimbi la wahamiaji haramu nchini, Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera imeendelea na Misako na Doria katika maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya hiyo.
Kufuatia Doria na Misako hiyo Novemba 23 mwaka huu wamekamatwa jumla ya Wahamiaji haramu 39 wengi wao wakiwa ni raia kutoka nchini Burundi walioingia Nchini kinyume Cha Sheria na taratibu za Uhamiaji.
Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Karagwe Mrakibu wa Uhamiaji SI Adinan Kidali Mussa ameeleza kuwa Misako hiyo ni endelevu na amewataka wananchi kuacha kushiriki kuwaingiza, kuwahifadhi Wala kusaidia kwa namna yoyote raia wa kigeni kukiuka Sheria za Uhamiaji na nchi kwa ujumla.
Idara ya uhamiaji inaendelea na Misako na doria muda wote Ili kuendelea kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Taifa Kwa Manufaa ya sasa na baadae.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime