Tanzania na Qatar zasaini makubaliano ya kutambuliana vyeti vya Ubaharia

London, Uingereza — Tanzania na Qatar leo  Novemba 24 mwaka huu wamesaini hati ya makubaliano (MoU) ya kutambuliana vyeti vya ubaharia, hatua inayotarajiwa kuongeza fursa za ajira na ushirikiano katika sekta ya usafirishaji baharini kati ya nchi hizo mbili.

Hafla hiyo imefanyika jijini London katika Hoteli ya The Dorchester, na kushuhudiwa na viongozi na wadau mbalimbali wa sekta ya bahari.

Kwa upande wa Tanzania, makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Malick Salum, huku upande wa Qatar ukisainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Abdulaziz Abdullah Al-Sulait.

MoU hii inatarajiwa kuboresha ubora, usalama na viwango vya utaalamu katika sekta ya ubaharia, sambamba na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na Qatar.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii