UN "Mwanamke mmoja aliuawa kila baada ya dakika 10"

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema kila baada ya dakika kumi mwanamke mmoja, mahali fulani duniani aliuliwa na mtu wa karibu, mwaka uliopita, huku ukilalamikia hatua dhaifu katika vita dhidi ya mauaji ya wana.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu dhidi ya Wanawake ilisema katika ripoti iliyotolewa katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake kwamba karibu wanawake na wasichana 50,000 waliuliwa na wenzi wao au wanafamilia mwaka wa 2024.

Ripoti hiyo ilisema asilimia 60 ya wanawake waliouawa kote ulimwenguni waliuliwa na wenzi au jamaa kama vile baba, wajomba, mama na kaka, tofauti na asilimia 11 ya wanaume waliouliwa na mtu wa karibu.

Idadi hiyo ya wanawake 50,000, imetokana na takwimu za nchi 117, imesema ripoti hiyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii